Sura 100 · Makkiya · 11 Aya
Sura Al-Adiyat
Farasi Wanaokimbia
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ
-
1
وَٱلْعَٰدِيَٰتِ ضَبْحًۭا
Wal'aadi yaati dabha
Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
-
2
فَٱلْمُورِيَٰتِ قَدْحًۭا
Fal moori yaati qadha
Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
-
3
فَٱلْمُغِيرَٰتِ صُبْحًۭا
Fal mugheeraati subha
Wakishambulia wakati wa asubuhi,
-
4
فَأَثَرْنَ بِهِۦ نَقْعًۭا
Fa atharna bihee naq'a
Huku wakitimua vumbi,
-
5
فَوَسَطْنَ بِهِۦ جَمْعًا
Fawa satna bihee jam'a
Na wakijitoma kati ya kundi,
-
6
إِنَّ ٱلْإِنسَٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٌۭ
Innal-insana lirabbihee lakanood
Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
-
7
وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌۭ
Wa innahu 'alaa zaalika la shaheed
Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
-
8
وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلْخَيْرِ لَشَدِيدٌ
Wa innahu lihubbil khairi la shadeed
Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
-
9
۞ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِى ٱلْقُبُورِ
Afala ya'lamu iza b'uthira ma filquboor
Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
-
10
وَحُصِّلَ مَا فِى ٱلصُّدُورِ
Wa hussila maa fis sudoor
Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
-
11
إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍۢ لَّخَبِيرٌۢ
Inna rabbahum bihim yauma 'izil la khabeer
Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!
Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil. Tafsiri na sauti kupitia huduma za bure za Al Quran Cloud / Islamic Network. Ufafanuzi kupitia Tafsir API huria.